•  Waigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamewaomba radhi watanzania kwa picha zao mbaya walizopigwa kwenye show za Fiesta.

     Wasanii hao wamezungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi  wa habari maelezo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuomba radhi kwa kupigwa picha hizo za nusu utupu walizopigwa kwenye show hizo.

     Wakiongena waandishi wa habari Aunty Ezekiel amesema ameumizwa na kitendo hicho kwakuwa wao kama wanawake katika jamii, wana wazazi, ndugu  jamaa, marafiki pamoja na mashabiki wao wanaowapenda na kuwaheshimu.

    Hivi karibu Aunty Ezekiel alijitetea na kunukuliwa kwenye chanzo kimoja akisema, “Ni kweli nilikuwa ninacheza katika Jukwaa (Stage) na nilikuwa nimekunywa, lakini sikuwa nimedhamiria kukaa uchi bali ni mbinu za wapiga picha ambao walitumia njia ya kuamua kunidhalilisha kwa kunipiga picha wakiwa chini ya Jukwaa (Stage) ili wapate kuuza magazeti yao, hata ukiangalia picha zenyewe zimepigwa kiujanja sana.”

    Waigizaji hao waliongozana na katibu Mkuu wa shirikisho la filamu Tanzania, TAFF, Wilson Makubi.


  • Kama utakuwa umeshawahi kusikia au hukuwahi basi hii ni tyme yako ya kuweza kusikiliza single ya Shawn Corey Carter alias Jay – Z kwa jina la “Oh My God” ambapo kwenye verse ya tatu ameweza kuitaja nchini ya Tanzania.

    Hii ni single yake toka kwenye album yake inayokwenda kwa jina la Kingdom Come aliyoitoa mwishoni mwa mwaka 2006 ikiwa imetengenezwa na Producer Just Blaze.
    Hii hapa ndio verse ya tatu ya Jay-Z alipoitaja Tanzania kwenye huu wimbo wa “Oh My God“:

    [Verse Three]
    Now these baby ballers toy rappers
    Calling out my name to bring the boy backwards
    Shooting air balls at the basket
    What you call money I paid more in taxes
    I got crowned King down in Africa
    Down in Nigeria do you have any idea
    Sold out shows in Seoul Korea
    Jo-berg, Dublin, Tanzania
    Lunch with Mandela, dinner with Cavalli
    Still got time to give water out to everybody
    Everybody fall back
    Y’all rapping I’m reenacting
    CNN you see it’s accurate
    ESPN see me in action
    Monday nights when the half ends
    When you ten years in holla back then


  • WAKATI watanzania wakiwa wamechoka na matukio machafu yanayofanywa na wasanii kwa kuacha nyeti zao nje, tukio lingine kama hilo limetokea tena kwa msanii ambaye watu hawakutarajia Nakaaya Sumari ambaye naye ameamua kuziweka nyeti zake hadharani kwa kutovaa nguo ya ndani, kitu ambacho kimempa aibu nzito.

    Tukio hilo limetokea hivi karibu wakati msanii huyo akiwa kwenye mahojiano na moja ya chombo cha habari, ambapo katika mkao ambao alikuwa amekaa alikuwa hajajifunika hata kitambaa wakati akijua wazi kuwa hajavaa nguo ya ndani ambayo kwa namna moja ama nyingine ingeweza kuficha aibu hiyo nzito ya kuziweka wazi nyeti zake.

    Tukio hilo limechukua sura mpya kwa wadau wa muziki wa kizazi kipya, kwani msanii huyo hakuwahi kufanya tukio la aibu kama hilo, ambalo limemchafua kwa kiasi kikubwa.